Monday, May 21, 2018

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU


 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa kwa makundi ya watu wenye ulemavu kwa mkoa wa Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Tasisi ya  Humanity  Action For Children Foundation,Rashid Mchujucko akizungumza mara baad aya kukabidhi Vifaa kwa makundi ya watu wenye ulemavu wa mkoa wa Dar es Salaam

Mjumbe wa Bodi wa Tasisi ya  Humanity  Action For Children Foundation,Haji Janguo akikabidhi Magongo ya kutembelea kwa watu wenye ulemavu wa viungo  wa mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Sabrina Semsimba  huku wajumbe wengine wakishuhudia 
 Msanii wa filamu nchini , Faiza Alli akizungumza juu ya umuhimu wa kujitolea kwa watu wenye mahitaji maalum hili kuleta usawa katika jamii.
 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah  akimvesha Kofia Mmoja ya Watoto wenye Albinism waliopata msada wa kibaiskeli cha kutembelea

 Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilaya ya Kinondoni , Sabrina Semsimba akishukuru mara baada ya kupokea Vifaa kwa ajili wenyeulemavu wa Viungo
 Mmoja ya Walemavu wa Macho akitoa neno la shukrani kwa ajili ya Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation
Baadhi ya Walemavu wa Macho wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa Fimbo za kutembelea na Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation

WIKI YA UBUNIFU YAANZA LEO KATIKA KUMBI ZA COSTECH JIJINI DAR ES SALAAM


 Kiongozi wa HDIF, Tanzania,David McGinty  akizungumza na Wahariri  na Wahandishi wa Vyombo Mbalimbali vya habari pamoja na wadau wa Masuala ya Sayansi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu kwa Vijana inayofanyika katika Kumbi Mbalimbali za Costech Jijini Dar es Salaam chini ya ufadhili wa UKAID na HDIF.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Dk Amos Nungu akizungumzia juu ya wiki ya Ubunifu kwa Vijana iliyoanza katika Kumbi mbali mbali za Costech ambapo wanufaika wataonesha kazi zao kwa kuwasilisha katika makongamano yatakayokuwa yanaendelea  chini ya ufadhili wa HDIF kwa kushirikiana na UKAID
Naibu Kiongozi wa HDIF Tanzania, Joseph Manirakiza akieleza namna HDIF ilivyoweza kutoa ruzuku kwa wanufaika wa miradi mbalimbali ya ubunifu wakati wa ufunguzi ya wiki ya ubunifu inayoendelea katika kumbi mbalimbali za COSTECH.
Baadhi ya wanufaika wa Mradi huo wakifatilia kwa ukaribu hottuba mbalimbali zinazotolewa na wadau wa masuala ya ubunifu.
Mtaalamu wa Masula ya Mawasiliano kutoka HDIF , Hannah Mwandoloma akiw apamoja na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mawasilisho juu ya wiki ya Ubunifu.
Wanufaika wa Wiki ya Ubunifu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa COSTECH, HDIF na UKAID


WAZIRI MWAKYEMBE AKABIDHI MAGARI FAINALI YA SHIKA NDINGA YA EFM TANGANYIKA PARKER'S

 Waziri wa Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kuhitimisha fainali za shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv , Kwa kuwapongeza kuwa kituo cha kwanza kuwakumbuka wasikilizaji wake kwa kuwawezesha kuwa Wajasiliamali.
 Waziri wa Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akikabidhi zawadi ya Gari kwa Mshindi wa shindano la Shika Ndinga kwa Wanaume ambaye ametokea mkoa wa Tanga.
 Waziri wa Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe  akikabidhi Zawadi ya Gari kwa Mshindi wa Shika Ndinga kwa Wanawake ambaye anatokea Mkoa wa  Mwanza

 Meneja wa Kituo Cha Radiio cha EFM na Tv E ,Dennisi Busulwa(Sebo) akizungumza na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika kushuhudia fainali za shindano la Shika Ndinga katika Viwanja vya Tanganyika Parker's Dar es Salaam.
 Watangazaji wa Kipindi cha Ubaoni kutoka Radio ya Efm, Mpoki na Dokii wakishangilia na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika fainali za shindano hilo katika Viwanja vya Tanganyika Parker's
 Washiriki wa Shindano la Shika Ndinga kwa Wanawake  wakiwa katika harakati za kujaza Vikombe katika hatua ya kwanza ya shindano hilo.


Majaji wa Shindano la Shika Ndinga wakiwa wamesimama tayari kwa ajili ya kutizama mchezo utakavyoendelea uwanjani
 Washiriki wa Kiume wakiwa katika hatua ya Mwisho ya kushika ndinga hili waweze kutwaa gari kwa atakayebaki mpaka mwisho
 Mmoja ya Washiriki kutoka mkoa wa Mtwara aliyotolewa katika hatua ya kwanza akitoa machozi mara baada ya kuenguliwa kwenye shindano.

Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifatilia shindano la Shika ndinga.

VIJANA WATAKIWA KUSIMAMA KIIMANI HILI KUFIKIA MAFANIKIO

Na Humphrey shao, Globu ya Jamii
Wito umetolewa kwa Vijana kutanguliza ibada kwanza katika shughuli zao za ujasilimali hili waweze kupata mafanikio ya kweli katika maisha .

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma alipokuw aakizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wanaojihusisha na masuala ya ujasiliamali chini ya Tasisi ya Her Initiative .
“ni Vizuri kongamno hili limefanyika katika mwezi huu mtukufu kwani Vijana wengi mnaingia katika biashara na kumsahau Mungu hali inayosababisha kuyumba kimaisha” amesema Vuma.
Ametaja kuwa swala Imani lina nafasi kubw akatika maisha ya Vijana kwani itasaidia kupunguza baadhi ya anasa amabzo zinapelekea kula mtaji wako wa baishara.
Amesema tatizo tulilonalo vijana wengi wetu atujui umuhimu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe lakini ni wepesi kuweka bando hata la 30,000 hili mradi usikosekane facebook wala Whats Up.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma  akizungumza wakati wa Kongamano la tatu la Panda katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Jijini Dar es Salaam ambapo Tasisi ya Her Initiative iliandaa  kongamano hilo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
 Msanii  wa Muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux akizungumza na Vijana wa Chuo Kikuu katika Tamasha la Panda TUDARCO. 
 Mnzilishi wa Mon Finance, Monica Joseph akieleza umuhimu wa kutunza akiba kwa Vijana hili waweze kufikia mafanikio.
 Mtangazaji wa Radio , Meena Ally  akiongoza mjadala wakati wa kongamano la Panda. 
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma  akikabidhi cheti kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya ujasiliamali.
Sehemu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu waliofika katika kongamano la Panda lililofanyika  Chuo Kikuu cha Tumaini 

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...