Thursday, June 7, 2018

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi na wagonjwa wa hospitali ya CCBRT mara baada ya kumaliza kutembelea hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Luke Maulid mwenye umri wa miaka 4 kutoka Mtwara ambaye anapata matibabu ya mguu katika hospitali ya CCBRT.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bibi Helena Mjinja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Musoma anayepata matibabu ya Fistula katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Watoto wanaocheza mpira huku wakiwa wanatumia miguu Bandia
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanawake ambao wamepata matibabu ya Fistula na kupona na kisha kufundishwa kazi za mikono katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.


ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA Na Mwandishi wetu 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.
Kamishna Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

Ni vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.
Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Bw. Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es salaam.”
“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akionesha zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

Tuesday, June 5, 2018

NCHI ZA NORDIC ZALIZISHWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI KWENYE MAPAMBANO YA RUSHWA

 Mkurugenzi wa Repoa, Dk.Donald Mmari akizungumza wakati Mjadala alikuwa akiongoza juu ya Mazingira ya Biashara nchini katik maadhimisho ya Wiki ya Nordic ambapo kwa asilimia kubwa wa wachangiaji wa mjadal huo wameipongeza Serikali ya Awamu ya tano kwa kuweza kuweka Mazingira wezeshi kwa wafanyabishara nchini na wawekezaji.
Balozi wa Denmark Nchini  Tanzania, Einar Jensen akizungumza jinsi alivyoridhishwa na mapambano dhidi ya rushwa yaliyofanyw ana Serikali ya awamu tano kw akukomesha rushwa sehemu za kazi na kuwabna mafisadi hasa katika eneo la bandari kiasi cha kuchangia ukuaji wa Biashara na uwekezaji nchini.
 . Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye akizungumza wakati wa Mjadala kwenye mkutano wa Changamoto zinazozikumba sekta binafsi uliondaliwa na Repoa , amapo alipata kueleza ni namna gani serikali ya awamu ya tano ilivyoweka mazingira wezeshi kwa wafanyabishara kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Repoa Dk . Donald Mmari 

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Nchini(TNBC), Raymond Mbilinyi  akizungumza ju ya baraza hilo lilivyoweza kusaidia kushawishi serikali kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini.
 Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Pekka Hukka katikati akitoa neno la ukaribisho kwa wadau waliofika katika mjadala wana namna Mazingira ya Biashara yalivyo nchini ikiwa kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya  Nchi za  Nordic
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni shauri ya Ujenzi Tanzania(COWI TANZANIA), Anne Mette Benzon akizungumza na wakati wa Mjdala huo ambapo alizungumzia hali ilivyo kwa wandisi Majenzi na Wakandarasi nchini walivyoweza kusaidia katika ujenzi na utunzaji wa Mazingira.
 Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya State Oil Tanzania, Genevieve Kasanga akieleza namna kampuniyake ilivyowekeza katika uchimbaji wa gesi na kuweza kuw ana mchango katika utunzaji wa Mazingira.
 Mkurugenzi wa Repoa, Dk.Donald Mmari aizungumza wakati wa ufunguzi wa Mjdala wa wiki ya Nchi za Nordic hapa nchini Tanzania walikaa kushoto na kulia ni mabalozi wa nchi hizo.

sehemu ya wadau walioshiriki mjadal wa wiki ya nchi za Nordic ju ya hali ya Mazingira ya Biashara nchini katika serikali ya awamu ya tano .

Monday, June 4, 2018

BENKI I&M YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA KUWAPA UJUMBE MZITONa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Benki ya I&M imeandaa futari Maalum kwa ajili ya wateja wake wa Dar es Salaam katika kuadhimisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa futari hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed amesema kuwa anawashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wa kibiashara ambao umeifanya benki hiyo kuendelea kusimama vyema.

“Mwezi wa Ramadhani unajulikana kama moja ya kati ya nguzo za Dini ya Kislamu na Benki ya I&M kwa kutambua umuhimu wake katika Jamii imeandaa futari hii kama sehemu ya matendo yanayopaswa kufanywa na wanajamii katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani” Amesema Baseer

Baseer  amesema kuwa benki itaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibishara wa mwaka 2018 na kuhakikisha kuwa inaendelea kupata ukuaji ni endelevu na kutaja kuwa wamejipanga kuanzisha huduma mpya ya pamoja na kutanua wigo wetu wa utoaji huduma kupitia njia mbadala za utoaji wa huduma za kibenki. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki I&M Baseer Mohamed akizungumza na Wateja wa benki hiyo waliofika katika futari iliyoandaliwa na Benki yake katika Mwezi hu Mtukufu wa Ramadhani
  Mkurugenzi wa bodi ya Benki I&M,Alan Mchaki  akitoa neno la Shukrani kwa  wateja waliofika katika futari hiyo


 Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja Ndabu Swere akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya huduma za benki hiyo katika kipindi cha mwak 2018.

Sehemu ya Wateja wa Benki ya I&M Wakifatilia hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo
 Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
 Wateja wa Benki I& M wakipakua futari mara baada ya swala katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki I& M wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya  futari katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

KUMBILAMOTO AZINDUA KISIMA CHA MAJI SHULE YA MSINGI KOMBO VINGUNGUTI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala  na Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto  amekabidhi kisima cha maji , Tofali na Mifuko ya Saruji katika shule ya msingi Kombo  ilyopo maeneo ya  kata ya Vingunguti na .


Akizungumza katika makabidhiano hayo  kumbilamoto amesema, ameamua kuchimba kisima hicho katika  shule ya msingi kombo kwa kuwa nimoja ya shule za sikunyingi  lakini imekuwa na tatizo la maji  kwamuda mrefu  ambapo watoto na walimu walikuwa wanapata shida jambo ambalo lilikuwa lina hatarisha afya zao nayeye baada ya kutembelea na kujionea shida hiyo alistushwa na kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo.

Amesema ,Kisima hicho kina uwezo wa kuhudumia wanafunzi wote wapatao 3000, na kuwa shukuru wafadhili walimsaidia kuchimba kisima hicho .

’Namshukuru sana Balozi wa Kuwait kwa msaada huo nilipo waeleza shidayangu kuwa nahitaji wani saidie kuchimba kisima katika shule hii hawakusita walinikubalia na sasa kisima kimekamilika kama unavyo ona hapa wanafunzi wanafurahia  maji  ‘’Alisema 

Katika hatua nyingine  Kumbilamoto ameanza kujenga ukuta katika shule hiyo baada ya kuombwa na walimu wa shule hiyo kwani ukuta ulipo unahatarisha maisha ya wanafunzi kuwa  unatikisika hivyo umekosa uimara.

‘’ Ukuta huu nataka niujenge upya na sehemu zingine niuongee urefu ili wanafunzi wanaruka wasiweze nihatari kwa maisha yao nimeonyeshwa na mwalimu mkuu wanafunzi wanaruka hawaelewi lakuambiwa  wanaweza kukutwa na majanga iwapo tutauacha hivi ,tayari haya matofari na mifuko hii nimekabidhi na ujenzai utaanza mara moja, ‘’ alisema .

Kwaupande wao   Walimu na wanafunzi  kataika shule ya msingi Kombo wamemshukuru   Kumbilamoto kwa kuchimba kisima  cha maji katika  katika shule hiyo kwani wameteseka kwa muda mrefu hawakuweza kupa msaada .

‘’Namshukuru sana Mstahiki Meya kwa kutujali kwakweli hali haikuwa nzuri watato walikuwa wanapata shinda sana maji ya kunywa na maji ya chooni na hata bustanizetu hapa zilikauka lakini sasa mabo nimazuri kama unavyo ona zimekuwa za kijani  tunaombatu sasa watuongezee matank  Mungu amzidishie,’’ Alisema mwalimu mkuu  Stella Mhando.

Naye  mwakilkishi wa  Afisa elimu wa manispaa ya iala katika hafla hiyo, Abdillahi  Magoti  Mchiya  amesema,  msaada huu umekuja wakati mwafaka na wanafunzi sasa watakuwa salama kwakuwa na maji ya kuaminika wataepukana ma magonjwa ya kuambukiza.

Picha za matukio mbalimbali katika uzinduzi wa kisima cha shule ya Kombo Vingunguti
 Naibu Meya wa Manispa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Omary Kumbilamoto akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Kisima Cha Maji katika shule ya Msingi Kombo Kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Stella Mhando.
 Diwani wa Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Waandishi wa Habari mara baad aya kufungua kisima hicho.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akifungua maji mara baada yakufanya uzinduzi wa kisima hicho
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumnbilamoto akikabidhi Tofali na Saruji kwa kamati ya shule ya Msingi Kombo iliyopo Vingunguti Dar es Salaam
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kombo kata ya Vingunguti wakifurahi mara baada yakupata Maji

WALINZI WA HIFADHI WATAKIWA KUWA MAKINI NA WADILIFU KUTOKANA NA WANYAMA KUTOKA NJE YA HIFADHI


Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii

WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo.

"La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society  ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika  eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game    Tracker Safaris  (TGTS).

Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.

Katika ziara hiyo TAWA  imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa  makampuni ya uwindaji wa kitalii zilizowekeza katika maeneo yao.

Maeneo yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja  na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Makao wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.


Dk Wakibara alisema, licha  mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo  ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa  takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.


Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159   vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini.


"Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema


Alisema kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi kufikia dola 80.


"kuna dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo  kiwango cha kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya kimataifa"alisema


Mwenyekiti wa bodi ya TAWA, Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka hiyo ipo katika mabadiliko  makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya maji, afya Elimu na uhifadhi.


Mwenyekiti huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko, Akikagua Gwaride la Askari wa Wanyamapori wa pori la akiba Maswa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa Wizara  ya Maliasili washirika wake

WAZAZI WAFURIKA KARIAKOO KUNUNUA NGUO ZA SIKUKU YA IDD EL FITRI

 Sehemu ya Wakazi wa Dar es Salaam wakichagua nguo za watoto katika Mtaa Congo Kariakoo wakichagua nguo za Sikuu katika msimu huu wa sikukuu ya Ramadhani.
 Wazazi wawili wakishauriana kuchagua nguo ipi inafaa kwa watoto wao kama walivyonswa katika Mtaa wa Congo na Agrey Kariakoo
Umati wa watu uliojazana Mtaa wa Congo Kariakoo kununua nguo za sikuu kwa ajili ya watoto wao katika msimu huu wa siku kuu ya Iddi  El Fitri

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...