Thursday, June 14, 2018

KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUWA KIPAUMBELE KATIKA KUCHOCHEA MAENDELEO Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo  jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya Maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na kuikabidhi.

Miradi aliyoitembelea Kubenea ni wa ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu sh. Milioni 7.7, miradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17, mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. Milioni 12 pamoja na ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.

Akizungumza baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea alisema ni vyema kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama.

"Mimi sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya wananchi....ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea alifanya kitu fulani.

"Kwahiyo niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu Chadema...tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu," alisema Kubenea.

Kubenea aliongeza kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya Hospitali, shule yanahitaji kuboreshwa.

Akizungumzia miradi hiyo Kubenea alisema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.

Akitoa shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha Mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mavurunza alisema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.

"Kwasasa tunafanya kazi kwa uhuru na usiri kati ya mgonjwa na daktari....tunakushukuru Mbunge wetu ambaye uliamua kujitolea fedha hizi kutoka katika mfuko wako," alisema Dorothy.

Aidha Dorothy alisema Zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  jengo la wazazi kuhitaji ukarabati, kutokuwa na uzio pamoja eneo hilo kuhitaji kusawazishwa ambapo Kubenea aliahidi atalisawazisha kwa kipindi kifupi.

Naye Mkuu wa Shule ya Mabibo, Hussein Mabibo alisema fedha zilizotolewa ambazo ni sh. milioni 17 zimesaidia kujenga madarasa matano, kubadilisha vigae vilivyochakaa na kuweka mabati, kupanga rangi shule, kukarabati ofisi ya walimu pamoja na ofisi ya mwalimu Mkuu.

"Tunakuamini wewe Mbunge wetu ukisema hua unatekeleza, hivyo tunaomba utusaidie pia kukamilisha maktaba, ujenzi wa uzio wa shule kwaajili ya usalama wa wanafunzi pamoja na ukarabati wa madarasa tisa ambayo yako katika hali mbaya," alisema Dady.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Soko la Mabibo, Yusuph Kilema alisema kisima kilichojengwa katika soko hilo kimekamilika kwa asilimia 90 ambapo bado vitu vichache ili kianze kutumika rasmi. Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo
 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea  akiwa amembeba mmoja wa watoto waliofika kupata huduma katika Zahanati ya Mavurunza .
 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo
 Mhandisi wa maji wa Manispa ya Ubungo akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea wakatia  alipotembelea miradi iijengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.
 Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.
 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akiwa ameongozana na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wafanyabishara wa soko la Mabibo
  Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.
  Mmoja ya wakazi wa Mavurunza akitoa pongezi kwa Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea mara bada ya kutekeleza ahadi zake kwa wakazi wa eneo hilo 

 wakazi wa Ubungo kata ya Mavurunza wakiwa wanasikiliza hotuba ya mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea 

 Mbunge wa jimbo la  Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwawa Mabibo

Wednesday, June 13, 2018

PICHA MBALIMBALI ZA HALI YA MASOKO JIJINI DAR ES SALAAM

 Muuzaji wa Ndizi katika soko la Buguruni akimuhudumia mmoja wa wateja waliofika kutaka huduma kama alivyokutwa na mpiga picha wetu
 Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akichagua mihogo kwa ajili ya futari kama alivyokutwa katika soko la Buguruni  
 Mchuuzi wa  Machungwa akiwa amebeba katika Tenga tayari kwa kwenda nayo mtaani kwa kutafuta wateja kama alivyokutwa katika mitaa ya Ilala Boma.

Wakazi wa Mbezi Mwisho Jijini Dar es Salaam wakisubiri usafiri wa kwenda mikoani katika kituo cha Stand Mpya ya Mbezi kwa sasa hali ya usafiri wa kwenda mikoani umekuwa wa shida kutokana na watu wengi kwenda likizo ya sikukuu.

JOHN AKHWARI VISITS UBA TANZANIA

1528811802949_IMG-20180611-WA0024
From Left Mr. Mathias Ninga, HR Business Partner East and Southern Africa UBA Group, next is Mr. Emeke Iweriebor, Executive Director East and Southern Africa UBA Group, next is the Renowned Olympian Mr.John Akhwari and Right is Mr.Usman Isiaka the Managing Director UBA Tanzania.
1528811804753_IMG-20180611-WA0027
Mr. John Akhwari stressing a point during his visit to UBA Tanzania. On his right hand is Mr. Emeke Iweriebor the Executive Director East and Southern Africa UBA Group.
1528811806107_IMG-20180611-WA0032
UBA Staff members pose with Mr. John Akhwari during his visit to UBA Tanzania Head Office.
1528811807227_IMG-20180611-WA0031
...................................................................................
On 29th May 2018, Lucky United Bank for Africa - Tanzania staff were visited by a legendary figure from the summer Olympics of 1968, Mr. John Steven Akwari who is famous for his quote "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race."
Executive Director Emeke E. Iweriebor was pleased to host Mr. Akhwari,s as he always referred to his story to motivate the team to making success stories through resilience and commitment.
The ED/RCEO charged all staff members to be strongly committed and positively inclined to creating a difference.
He urged staff to become believers, be resilient and always go the extra miles to achieve exceptional results.
During his dialogue, the ED/RCEO largely used the example of John Steven Akhwari a marathon runner during the 1968 Olympic games in Mexico City. Akhwari was a world class runner of the 1960’s and 1970’s where he participated in different Olympic games across the world. His 1968’s Olympics in Mexico is regarded the most heroic story to date.
This is because during his 42 Kilometre marathon mission Akhwari was Cramped up due to the high altitude of the city. He had not trained at such an altitude back in his country. At the 30 -kilometre point there was jockeying for position between some runners and he was hit. He fell badly wounding his knee and dislocating that joint plus his shoulder hit hard against the pavement.
He however continued running, finishing last among the 57 competitors who completed the race started by 75 runners.
The winner of the marathon was Mamo Wolde of Ethiopia who finished in 2:20:26. Akhwari finished in 3:25:27 one hour later when there were only a few thousand people left in the stadium, and the sun had set and television crew sent out.
As he finally crossed the finish line a cheer came from the small crowd. When interviewed later and asked why he continued running, he said, "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race."
During his engagement with UBA- Tanzania staff Mr. Akhwari reminded the agile audience that he did not finish the race to prove a point but simply to ensure that he finished what he was set to do.
Managing Director UBA - Tanzania honoured the iconic figure and urged his staff to always be the first to do things differently saying “the historical moment demonstrates resilience, consistency and Focus the ultimate goal must be achieved regardless the circumstances and strive to complete what is started and not rely on obstacles as excuses”.
He said each individual is born with an inner talent and it is important to let shine the talent and become more productive than being timid and live without achieving significant results.
During the 1968 race, Akhwari’s body was exhausted but not his spirit; his competitors crossed him one by one but his determination rewarded him in tremendous pain. Akhwari never won any Olympic gold medal but he became the greatest example of never-give-up spirit, and a tale of courage and his story has widely been told across the world especially in education institutions.
John Stephen Akhwari has been honoured and symbolized as the living example of courage and determination. In 1983, he was awarded a National Hero Medal of Honour. In 2000, he was invited to the Olympics in Sydney, Australia and 2008 he was invited in Beijing as a goodwill ambassador to inspire the Olympic athletes for the 2008 Games.

Tuesday, June 12, 2018

Jafo Aagiza Uanzishwa Wa ‘One Stop Center’ kwa ajili ya Wawekezaji

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya Nchini kuhakikisha wanaanzisha kituoa kimoja cha huduma ‘One Stop Center’ kwa ajili ya wawekezaji.

Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya namna ya Uendeshaji wa  Mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote Nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
Katika Warsha hiyo inayowajumuisha viongozi wa Ngazi za Mkoa na Wilaya Mhe. Jafo amesema mazingira magumu ya upatikanaji wa taarifa za uwekezaji na urasimu uliopo katika Mikoa na Wilaya ndio unaowakwaza Wawekezaji katika harakati zao za kutaka kuwekeza katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Imekuwa ni vigumu sana kwa Muwekezaji kupata taarifa sahihi na kwa wakati katika maeneo yetu na hii imekua ikiwakatisha moyo na kupelekea hata kusitisha mpango mzima na nia yao ya kuwekeza katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, inatakiwa tubadilike na tuweke mazingira rahisi yatakayomuweza kila mdau anayetaka kuwekez kupata taarifa anazozihitaji kwa urahisi.

Hali hii inarudisha nyuma juhudi zetu za kuhamasisha uwekezaji sasa basi kila kiongozi wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanaanzisha kituo kimoja “One Stop Center” ambacho kitatoa huduma zote kwa Wawekezaji kama vile upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji, Leseni za biashara, Hati miliki, usajili wa kampuni, namna ya ulipaji wa kodi nk” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa warsha hii imewakutanisha wadau kutoka Sekta ya umma na binafsi katika kila ngazi ya utawala ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji Nchini na hivyo basi ni wakati wa kukubaliana kwa pamoja namna mabaraza ya Biashara yatakavyosaidia katika kukuza Uchumi wa Viwanda ambao ndio muelekeo wetu kama Taifa kwa hivi sasa.

Sambamba na hilo Jafo aliwakumbusha viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa pamoja na majukumu mengine wanapaswa kutengeneza mazingira bora ya kufanyia biashara na uwekezaji, kuibua fursa za uwekezaji, kuzinadi fursa zilizoibuliwa kupitia Makongamano ya uwekezaji na kuandaa midahalo mahususi.

Pia Mhe. Jafo alisisitiza kuwa mara baada ya kikao hiki kila kiongozi akahakikishe kuwa Vikao vya mabaraza ya Biashara vinafanyika kwa mujibu wa Sheria na viongozi washiriki katika vikao hivyo na maazimio ya vikao hivyo yakashughulikiwe kwa wakati na kutoa mrejesho kwa upande wa sekta za umma na binafsi.

Aidha kila Halmashauri zikatenge bajeti kwa ajili ya uendeshaji wa Mabaraza ya biashara  na kwa upande wa Sekta binafsia ziandae utaratibu mzuri wa kuchangia gharama za uendeshaji wa vikao hivyo.

Alimalizia kuwa Mradi wa LIC kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Baraza la Taifa la Biashara kuandaa utaratibu wa kueneza uzoefu uliopatikana katika Mikoa miwli ya Dodoma na Kigoma ambapo mradi huu umetekelezwa ili mikoa mingine iweze kujifunza na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
Mabaraza ya Biashara Tanzania yameanzishwa kwa mujibu wa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 691 la tarehe 28 Seot,2001.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akifungua warsha ya kujadili changamoto za Uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara Tanzania inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akizungumza na wadau wa baraza la biashara kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa OR-TAMISEMI Beatrice Kimoleta(kwanza Kushoto) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala bora na Huduma OR-TAMISEMI Angelista Kihaga (kwanza kulia) pamoja na wadau wa Baraza la Biashara katika warsha ya kujadili uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara.
1.      Mkurugenzi Msaidia wa Utawala toka OR-TAMISEMI Bw. Mrisho Mrisho akiongoza warsha ya Mabaraza ya Biashara Tanzania.

1Mshauri wa Majadiliano baina ya Sekta Umma na Binafsi wa LIC Bw. Donald Liya (Kwanza kushoto) akifuatiwa na Kiongozi Msaidizi wa Timu ya LIC Bw. Peter Laizer, Mshauri wa Mradi wa LIC toka Taasisi ya Sekta Binafsi Bi. Rehema Mbugi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA Bw. Gotfried Muganda wakifuatilia warsha ya kujadili changamoto ya Uendeshaji wa Mabraza ya Biashara.

Monday, June 11, 2018

KESI YA UCHOCHEZI YA KINA MBOWE KUENDELEA KESHO MAHAKKAMA YA KISUTU

 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuamuru upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabikili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake nane kufanyia  marekebisho katika hati ya mashtaka.


Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo leo  Juni 11 baadabaada ya kupitia mapingamizi nane yaliyowasiĺishwa mahakamani hapo na mawakili wa utetezi, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya.

Hata hivyo, kufuatia uamuzi huo Wakili, Kibatala alieleza kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Katika Mapingamizi hayo, upande wa utetezi waliiomba mahakama yanayowakabili kuyafuta mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa sababu yana mapungufu kisheria ikiwamo shtaka moja kuwa na makosa mawili na washtakiwa waachiwe huru.

Ombi mbadala wa hilo, Kibatala aliomba iwapo mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria.

Hata hivyo, wakili Faraja Nchimbi akisaidiana na, Paul Kadushi walipinga madai hayo na kudai kuwa hayana mashiko kisheria.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri aikubaliana na baadhi ya hoja za upande wa utetezi, moja wapo ikiwa katika shtaka la pili, tatu, nne, tano, sita na saba yanamapungufu kisheria na kuamuru upande wa mashtaka kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.

Baada ya kutoa uamuzi huo, wakili Kibatala aliieleza mahakama kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo hivyo aliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa

Wakili   Kibatala alidai kuwa wanakata rufaa kwa sababu wao waliomba mashtaka hayo yafutwe lakini mahakama imeona imeamuru kuwa yafanyiwe marekebisho licha ya kuona kuwa kweli mengine ni batili.

Baada ya Kibatala kueleza hayo, wakili wa serikali Paul Kadushi alidai kuwa uamuzi uliotolewa wa kifanyia marekebisho hati ya mashtaka ni uamuzi mdogo ndani ya kesi, na kwa mujibu wa sheria uamuzi mdogo ambao hauwez kumaliza kesi kama huo hawawezi kuukatia rufaa.

Kibatala alisisitiza kuwa kwa kuwa mahakama imeona mashtaka hayo ni batili,  mashtaka hayo yanakufa ndiyo maana mahakama ikaamuru Marekebisho hivyo watakata rufaa.

Baada ya mabishano hayo ya kisheria, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo atatoa uamuzi kama inaridhia ombi la akina Kibatala kukata rufaa ama la.


Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo Namba 112 ya 2018 ni  mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Mbunge wa Tarime mjini
Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk  Vicenti  Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.


Katika shtaka moja wapo wanadaiwa kula njama, Februari Mosi 2018 na Februari 16, 2018. Wakiwa Kinondoni Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani kwa kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

 Viongozi wa CHADEMA wkitoka Mahakamani mara baada ya  shauri lao kuharishw ampaka kesho

RIDHIWANI APATA FUTARI NA VITUO VITANO VYA WATOTO YATIMA NYUMBANI KWAO MSOGA

 Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa ana swali kabla ya Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
 Mmoja ya Wadau kutoka Tasisi ya K Innovates Nasra Kaseja akizungumz ajuu ya umuhimu wa kuwasaidia watoto yatima wakati wa Iftar iliyoandaliwa na  Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
 Msherehesjai wakati wa Iftar hiyo Mtangazajoi wa Raidio Masoud Kipanya akizungumza juu ya utaratibu na umuhimu wa kufutirisha makundi ya watu maalum katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.  
 Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa ana swali kabla ya Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
 Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akipakuwa chakula wakati wa  Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
 Wadau wa Tasisi ya Ko Innoavate Pink Ijab wakiwa katika picha ya kabla ya Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
 Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete katikati  akiwa na Wadau waliotoa Vifaa kwa ajili ya Watoto Yatima wakati wa  Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar  hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
Baadi ya wadau waliofika  katika  Iftar   iliyofanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AIPONGEZA HOSPITALI YA MAMC-MLOGANZILA KWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA


Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka .

Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais aliutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu.

Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “ Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uunguzi na kujitolea malipo yetu yapo kwa mwenyezi Mungu”

Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) anayemfuatia ni Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa magonjwa ya dharula Dkt. Catherine Shali wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu,  Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo katika mashime ya MRI wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipanda ngazi za umeme.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulshoto) wakimsikiliza Mkuu wa Skuli ya Meno-MUHAS Dkt. Elison Simon wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akitoa maelekezo kwa Meneja wa Maabala Glory Mmbando wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa wakuu wa vitengo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Amani Ahmada mwenye umri ya miaka 6, wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza machache.
Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini.
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kutolea machache ufafanuzi.
Picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Picha ya pmoja na wafanyakazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza wananchi wanaopata huduma ya matibabu Mloganzila wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud akitolea ufafanuzi malalamiko ya wananchi wanaopata huduma katika hospitali ya Mloganzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupongeza ungozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila kwa juhudi wanazokabialiana nazo katika kutatua changamoto wanazokabilia nazo.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...