Friday, July 20, 2018

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondokaMwandishi wetu,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini, kujiandaa kuondoka ndani ya miezi mitatu kabla ya operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu kuanza.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika eneo la  hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Makao, wilayani Meatu, Dk Kigwangalla alisema wavamizi wa maeneo ya hifadhi wengi wamekuwa wakijihusisha na matukio ya ujangili.

"Utakuta kijiji kina ardhi kubwa, lakini wengine wanajenga hadi katika ndani ya eneo la mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na hao mara nyingi ndio wanaingiza mifugo hifadhini usiku na kufanya ujangili," alisema

Alisema maeneo mengi ya hifadhi na mapori ya akiba nchini yamevamiwa na wananchi jambo ambalo serikali haiwezi kukubali yaharibiwe ama kutumika kwa ujangili.

Waziri huyo, pia alitembelea kambi ya kitalii ya Mbono inayomilikiwa na Kampuni ya Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na hoteli ya kitalii ya Mwiba (Mwiba Lodge) na kushuhudia vikosi vya kupambana na ujangili katika maeneo hayo ambavyo vipo yapo chini ya taasisi  Friedkin Conservation Fund (FCF) na kueleza kuridhishwa na uwekezaji wa taasisi hiyo.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Mwiba Holding, Abdulkadir Mohammed, alisema katika eneo la Mwiba wamewekeza sh 2.2 bilion na hivi sasa wanaendelea na shughuli za uhifadhi na utalii.

"Mheshimiwa Waziri katika eneo hili, kampuni yetu inafanya utalii wa picha na kuna hoteli, tunafanyakazi kwa amani na utulivu na vijijini vinavyotuzunguka," alisema.

Mwenyekiti wa kijiji cha Makao, Anthony Philip, alimweleza Waziri Dk Kigwangalla kuwa, katika eneo hilo kuna mahusiano mazuri baina ya vijiji na wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa fedha.

Philipo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwangudo alisema kijiji cha Makao kimekuwa kikipata zaidi ya Sh 147 milioni kwa mwaka kutoka kwa mwekezaji na vijiji vingine sita vimekuwa vikipata zaidi ya milioni 80,000 kila mwaka.

Akiwa katika pori la akiba la Maswa, Meneja wa pori hilo, Lusato Masinde alisema pia wanauhusiano mzuri na wawekezaji ambao licha ya kulipia ada za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa huduma mbali mbali ikiwepo maji.

Hata hivyo, alisema katika pori hilo changamoto kubwa ni uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi    na upungufu wa vitendea kazi.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akipata Maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Mwiba  ambayo  ndiyo imewekeza katika wilaya hiyo ya Meatu, Abdulkadir Mohamed akitoa maelezo kwa Waziri Juu ya  mradi huo
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla a kipata Maelezo kutoka kwa Meneja wa Mwiba Lodge , Alina  Redka  juu ya sehemu ya kuangalzia Mbugani.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akikagua Gwaride la Askari wa Wanyamapori katika pori la akiba Meatu.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akiwa ameongozana na Wakurugenzi wa Kampuni ya Mwiba Holding Ltd inayofany auwekezaji katika pori la akiba Meatu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akipata Maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wafanyakazi wa Tanzania Game Trackers Safaris

Wednesday, July 18, 2018

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampuni ya Moja Spesho inayoenfdesha michezo ya kubahatisha.Ambapo amekabidhiwa kiasi cha shilingi Milioni Miambili na nne .
 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo  akiwa na mmoja ya wakurugenzi wa Kampuni ya Moja Spesho mara baada ya kumkabidhi Zawadi.
Mshindi wa Shindano la Moja beti, Rosemary  Luhamo , akikabidhiwa fedaha zake na kampuni ya Moja Spesho Kupita Benki ya CRDB

DED UBUNGO AFANYA UKAGUZI KATIKAUJENZI WA MADARASA MANNE YA KIMARA SEKONDARI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akizungumza jambo na kaimu Mwamlimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimara wakati alipoifika kukagua ujeni wa Madarasa Manne yanayojengwa katika Sekondari hiyo Mpya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo, akikagua ubora wa Zege linalotumika katika ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari Kimara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akisaidiwa kupanda  juu ya Msingi na Afisa Mtendaji wa kata Kimara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akitoa maelekezo kwa mkandarasi aweze kumaliza ujezni huo kwa wakati
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akiagana na walimu wa shule ya Sekondari Kimara

Tuesday, July 17, 2018

MANOTA APITA BILA KUPINGWA UCHAGUZI MDOGO KIMARA

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo, John Kayombo amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi wa Pascal Manota kuwa Mshindi katika Uchaguzi mdogo ulioitishwa nchini katika kata ya Kimara.
Kayombo  amemtangaza Manota kuwa Diwani Mteule kutokana na madiwani wengine kutoka vyama pinzani kushindwa kujibu hoja za mapingamizi aliyowawekea kama mapungufu wakati wa ujazaji wa fomu.
“Vyama vilivyoweza kuchukua fomu ya kugombea Udiwani katika Kata ya Kimara ni , Act Wazalendo, Chadema, Cuf na CCM lakini kutokana na Mapungufu yaliyojitokeza katika ujazaji wa fomu bwana Pascal Manota namtangaza kama Diwani Mteule aliyepita bila ya kupingwa”amesema Kayombo.

Kwa Upande wake Pascala Manota ambaye ni Diwani Mteule katika kata ya Kimara amewetaka wapinzani kuacha siasa za uongo za kuwasingizia watendaji kuwa ndio wanaharibu uchaguzi wakati wao ndio wa kwanza kuvunja taratibu za uchaguzi na sharia zilizowekwa.

Amesema kuwa wagombea wote walichukua fomu na zikajazwa na kubandikwa katika mbao ya matangazo kata hivyo baada ya kuona mapungufu ya wagombea wake aliamua kuwawekea mapingamizi hivyo kufuatia mapingamizi hayo wagombea wote wametupwa nje.

Amesema kuwa sasa anasubiri kuapishwa hili aendelee kuwatumikia wakazi wa kimara na hili waweze kupata maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo , John Kayombo ambaye pia ndio Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri hiyo akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo kuwa Ndugu Pascal Manota kapita bila kupingwa.
Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akisaini kitabu cha kupokea barua ya kuwa Diwani Mteule aliyepita bila kupingw akatika kata ya Kimara.
 Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akipokea barua ya kuwa Mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kupita bila kupingwa mara baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa mapingamizi
Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kutangazwa mshindi

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...