Tuesday, August 7, 2018

WASICHANA 10,000 WAFIKIWA NA TASISI YA MSICHANA INITIATIVE

Na Humphrey Shao, Globu jamii

Zaidi ya Wasichana 10,000 wamefikiwa na huduma zitolewazo na tasisi ya Msichana Initiative katika kipindi cha miaka Miwili na nusu tangu kuanzishwa kwake nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo , Rebeca Gyumi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kongamano la Ajenda ya Msichana linalo Taraji kufanyika Agosti 11 mwaka hu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.

Gyumi amesema kuwa kupitia kongamano hili jumla ya Washiriki 1000 watashiriki wakiwemo wasichana walio ndani ya shule na nje ya shule kutoka klabu za Msichana Café na Makundi ya watu wenye mahitaji maalum.

“kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa tasisi hii tumeweza kuwafikia wasicha 10000 moja kwa moja hivyo katika mkutano wa mwaka huu 2018 tumekuja na kauli mbiu isemayo ‘Nafasi ya Jamii kwenye kuunda na kutetea haki za mtoto wa kike’ huku msisitizo mkubwa wa kauli hii mbiu ni kuangalia namna gani  Wasichana wanazifahamu haki zao na kujua jinsi ya kuzitetea ili kuleta Mabadiliko chanya kwenye jamii” amesema Gyumi.

Gyumi alitaka kuwa mgeni rasmi katika kongamano hili anataraji kuwa Mkurugenzi kutoka shirika la Women Fund Tanzania(WFT)Mery Lusimbi,  aidha Wasichana watapata nafasi ya kuzungumzia changamaoto mbalimbali wanazozipitia .

Amesema tasisi ya Msichana Initiative ambayo inafanya kazi kwa ukaribu na serikali katika kupinga ndoa za utotoni , Unyanyasaji na ukandamizaji wa kijinsia  kwa lengo la kuwapa nafsi wasichana kufikia malengo yanayotakiwa katika Maisha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kongamano la Ajenda ya Msichacha linalotaraji kufanyika agosti 11 mwaka huu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kutambulisha Kongamano la Ajenda ya Msichana

DR MPANGO AWAPONGEZA AMANA BENKI KWA KAZI NZURI NA HUDUMA BORA KWA JAMII

 sa

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Tanga

Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango amewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kutumia fursa ya uwepo wa Amana Benki katika mkoa huo kama fursa ya kujipatia Maendeleo kutokana na benki hiyo kuwa na huduma ya mikopo isiyokuwa na riba.

Waziri Mpango amesema hayo  mkoani Tanga wakati alipokuwa akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo    katika mkoa huo.

 "nimefurahishwa na jitihada za Amana Bank katika kutanua huduma zake kwa wananchi wa mikoani. Vilevile, nimewasisitiza wana Tanga kutumia fursa waliyopata kutoka Amana Bank kwa kuwafikishia huduma za bank hiyo kwao,ikiwemo mikopo bila riba jambo ambalo litawasaidia sana kujiinua kichumi kwa kukopa na kurejesha kwa wakati"amesema Waziri Mpango. Akizungumza kwa niaba ya benki hiyo  Mkurugenzi wa Amana Benki Dk Muhsin Masoud, amesema Benki ya Kiislamu ya  Amana hapa nchini imefungua tawi lake jipya jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Benki hiyo kufikisha huduma zake kwa watu wa  mikoani.

amesema kuwa Benki hiyo inatarajia kufungua matawi yake mengine Zanzibar  na Dodoma hivi karibuni hili kuzidi kuwasogelea wananchi nakutaja kuwa  akaunti zinazopatikana katika Benki hiyo,  ni  akaunti ya akiba ya wanafunzi, akaunti ya akiba ya Hijja, akaunti ya akiba ya mtoto(nuru), akaunti ya akiba ya mwanamke(anisaa) na akaunti binafsi.

ametaja kuwa kwa sasa Benki hiyo ya Amana inafikisha jumla ya matawi 8, matano yakiwa Dar es Salaam, Moja Mwanza,Arusha na hilo la jijini Tanga. Amana Benki ilianzishwa mnamo Novemba 24, 2011 kwa lengo la kukidhi haja ya wateja wa kibenki nchini ya kupata huduma zinazozingatia misingi ya sharia za Kiislamu.

 Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango akiwa na Mkuu wa Mkoa Wa Tanga , Martin Shigela  wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi Jipya la Amana Benki Mkoani Tanga.

 Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango  akifunua kitambaa cha jiwe la Msingi wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Amana Benki Mkoani Tanga
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Martin Shigela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Amana Bneki katika mkoa wake
 Dk Muhsin Masoud,Mkurugenzi wa Amana Bank akielezea huduma zitakazotolewa katika tawi hilo la Mkoa wa Tanga.
 Waziri wa Fedha Philip Mpango akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wateja mashuhuri wa benki hiyo wa mkoa wa Tanga.
Waziri wa Fedha akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Viongozi wa mkoa wa Tanga.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...