Saturday, August 25, 2018

ABDUL Mteketa: Nimefika daraja la MAGUFULI kabla sijafa
Na. Mwandishi Wetu
-KILOMBERO
MBUNGE wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa (CCM), ametimiza azma yake ya kutembelea daraja jipya la Magufuli lililopo Wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza leo baada ya kutembelea daraja hilo, alisema yeye alikuwa ni moja ya viongozi waliopigania ujenzi wa daraja hilo ukamilike haraka wakati Rais Dk. John Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu.
“Kama unavyojua katika maisha yangu ya kuumwa pengine nisingeliona hili daraja. Lakini leo nimefika na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.


Abdul Mteketa akiwa katika daraja la Magufuli leo hii
“Watu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mpendwa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kulijenga taifa letu na kuleta maendeleo kwa kasi.
“…tayari umekamilisha ujenzi wa daraja na ameshaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Kidatu hadi Ifaraka- Ulanga, sasa ametufuta machozi watu wa Kilombero-Ulanga na kwa dhati ninampongeza Rais Magufuli,” alisema Mteketa
Akizungumza hali yake ya kiafya, alisema anamshukuru Rais Magufuli kwani kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kupata msaada wa matibabu.
“Awali nilikuwa na atembetea kwenye wheel chair  lakini kwa sasa ninaweza alau kusimama kwa msaada wa magongo.  Sina la kusema zaidi ya kusema asante Rais Magufuli nasi Watanzania tunakuombea kwa Mungu akupe afya njema ili uweze kuongoza taifa letu kwa upendo kama unavyofanya sasa,” alisema

Friday, August 24, 2018

WARAMI WAMVAA MBOWE WAMTAKA ASIIPANGIE KAZI MAHAKAMA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuishukia mahakama kuwa haimtendei haki, Watetezi wa Rasilimali za taifa Wasio na Mipaka (WARAMI) wameibuka na kupinga vikali kitendo hicho kwa kusema Mahakama aingiliwi wala aipangiwi hivyo ni vyema wakaicha ifanyekazi kwa weledi .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami,  Philipo Mwakibinga, alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe cha kulalamika kwa vyombo vya habari kuhusu kesi ambayo bado ipo mahakamani, ni fedheha na kuidhalilisha Mahakama.
Amesema Mbowe kupitia tamko lake alidai kuwa kuna viashiria ambavyo vinaonyesha kuwa mahakama inaingiliwa na dola huku akijua kwamba si kweli na kwamba mahakama ni mhimili unaotenda kazi zake kwa uhuru.
 “Si mara ya kwanza kwa Mbowe kuingilia uhuru wa mahakama hasa pale anapoona kuwa kusa analoshtakiwa nalo linaweza kumtia hatiani kwa mujibu wa sheria,” alisema Mwakibinga na kuongeza Mbowe anafanya hivyo kwa nia ya kupata huruma ya watanzania.
“Jana (juzi) kupitia tamko lake alisema kuwa dola inaingilia mahakama ili kuishinikiza yeye ashindwe. Utagundua kwamba huku ni kuvunja sheria na taratibu ambazo tumejiwekea. Tunafahamu kwamba suala lililopo mahakamani halipaswi kuzungumzwa katika public (hadharani) likiwa bado linaendelea mahakamani,” amesema Mwakibinga.
 amesema Mbowe kupitia vyombo vya habari alitoa kauli za uchochezi na kulitisha Taifa kwa kusema kuwa yatatokea yale yaliyotokea nchini Uganda.
“Kwanini Mbowe anatumia vibaya uhuru wake wa kujieleza, je anahaki miliki ya nchi hii? Kwanini ameanza kuitilia shaka mahakama kwamba haitamtendea haki,”
Amesema pamoja na Mbowe kudai kuwa wameonewa kuhusu sakata la kifo cha Mwanafunzi Akwilina ambacho kilitokea wakati wa maandamano yao, watu wanajua kuwa kifo hicho kilisababishwa na wao kwa mazingira yeyote.
“Mbowe ndiye aliyehamasisha watu kwenda kufuata barua za mawakala kwa maandamano tena yasiyo na kibali, lakini pia Mbowe amenukuliwa akisema kwamba wapo tayari kubeba majeneza zaidi ya 200, sasa yawezekana hilo jeneza moja lilikua kati ya hayo aliyosema,” amesema.
Amesema endapo Mbowe na wafuasi wao wasingeenda kufuata barua kwa maandamano hakuna machafuko ambayo yangetokea na kwamba kifo cha Akwilina kisingetokea.
“Ukijaribu kuangalia mwenendo mzima wa tukio hilo Mbowe anaona kabisa anayo hatia na ndiyo maana anakimbia na kusema anaonewa huku akilalama suala  la wakili wake kujitoa ambalo kimsingi ni kawaida endapo wakili anaona atafedheheka kutetea watu ambao wana hatia, alitaka wakili afanye nini?” amehoji.
“Hawa ndio ambao kwa miaka yote wamekuwa wakilalamika mahakama zetu zinachelewesha kesi, leo hii mahakama zimeongeza ufanisi na kujitahidi kusikiliza mashauri kwa haraka wao wanadai kesi inapelekwa haraka,” amesema .

Aidha alitoa wito kwa vyombo vya usalama nchini kumchukulia Mbowe hatua za kisheria kutokana na kutoa matamko ya kichochezi licha ya kuwa ni mshtakiwa wa kesi ya uchochezi.

Monday, August 20, 2018

UJUMBE KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA MANISPAA UBUNGO KUJIFUNZA JINSI YA KUENDESHA SERIKALI YA ZA MITAA

 Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao kazi na wajumbe wa kamati ya fedha na ugeni kutoka nchini Marekani uliokuja kijifunza jinsi  gani mfumo wa kuendesha Serikali za mitaa unavyofanya kazi  hapa nchini Tanzania
 Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akiongoza kikao cha Kamati ya Fedha mara baada ya kutembelewa na ujumbe Maalum kutoka nchini Marekani uliokuja kujifunza ni namna gani Tanzania inaendesha Serikali za Mitaa.
 Mwenyeji wa Vijana hao kutoka Marekani amabye ni Mtanzania akitoa maelezo juu ya ujio wa vijana hao katika bara la Afrika.
 Mmoja ya Vijana kutoka nchini Marekani waliofika Manispaa ya Ubungo Kijifunza namna mfumo wa Serikali za Mitaa unavyofanya kazi  hapa nchini akieleza jambo kwa  Wajumbe wa kamati ya fedha ya Manispaa hiyo
 Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akiwa katika picha ya pamoja na Wageni hao pamoja na Wakurgenzi wa Halmashauri hiyo.
 Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akiwa katika picha ya Pamoja ya Wageni hao na Wabunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akiw akatika picha ya pamoja ya wageni hao kutoka Marekani na Madiwani ambao ni wajumbe wa kamati ya fedha.

The think Tankers of Tanzania yapongez akasi ya utendaji wa Rais Dk John Pombe Magufuli

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 Uongozi wa Tasisi isiyo ya Kiserikali ya ‘The Think Tankers of Tanzania’ umesikitishwa na baadhi ya viongozi wateule ambao kwa kutafuta KIKI ana kutaja mambo makubwa saba katika utawala wa awamu ya tano unaonngozw ana Rais Dr John Pombe Magufuli.

Akizunguamza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katibu wa The Think Tankesr of Tanzania, Ibrahim  Jeremiah alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano  Katika upande wa Kilimo  imeweza kutekeleza mikakati mbalimbali inayoazimia kumuinua Mkulima wa Tanzania.

“ Ruzuku kwa pembejeo za kilimo kuondoa tozo za kodi na kuwatafutia masoko wakulima, kwa mfano wakulima wa Korosho mwaka jana waliuza Korosho mpaka Tsh 4000 kwa kilo lakini pia mwaka jana wakulima wa mahindi walifanikiwa kuuza mahindi mpaka kwa Tshs 1000 kwa kilo ya mahindi na mwaka huu pia Mh. Rais hajachoka kuwahangaikia wakulima wa Tanzania, Kikao chake cha siku chache zilizopita na Mkurugenzi na Shirika la mpango wa chakula (WFD) BW. DAVID BEASSLEY kuhusu kununua mazao ya chakula Tanzania kimepokelewa kwa furaha kuu mno na wakulima wa Tanzania” alisema Jeremiah  

Alisema kuwa katika awamu hii tumeshuhudia ufufuaji wa Shirika letu la Ndege ambapo ilikuwa ni aibu kubwa kwa Taifa kutokuwa na ndege, Ndege hizi haziishii tu kutuingizia mapato na kulitangaza Taifa bali zinasaidia kukuza sekta ya utalii na kuvutia wawekezaji, muwekezaji hawezi kumudu kusafiri umbali mrefu mfano toka Dare es Salaam mpaka Kigoma kwenda kufanya research au kuwekeza, ufufuaji wa usafiri wa Anga umeleta tija mno kwa Taifa.

“Sasa hivi watanzania tuna vitu vinne vinapaa angani, 3 – Bombardier na 1 ni Boeing wapo wanaoumia sana kusikia Tanzania inasonga mbele, nataka niwape taarifa itakayowaumiza kuwa mwezi uliopita tumeingiza Bilion 4.5 kupitia mapato ya ndege zetu na tunatarajia kuongeza ndege nyingine 5, Bombardier  Q400 2, Bombardier CS300 mbili, na Boeing 1 jumla tutakuwa na ndege 9”Alisema 


 katibu wa The Think Tankesr of Tanzania, Ibrahim  Jeremiah  akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mambo  mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano
 Mwenyekiti wa The Think Tankers of Tanzania,Piter Msaki akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamko la ubalozi wa Marekani

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...