Thursday, August 30, 2018

KUMBILAMOTO AENDELEA NA MIKUTANO YA KAMPENI KATIKA KATA YA VINGUNGUTI

 Mgombea Udiwani wa Kata ya Vingunguti Kupitia Chama cha Mapinduzi , Omary Kumbilamoto akizungumza  na Wakazi wa Mtaa wa Butiama Vinguti wakati wa Mkutano wake wa Kampeni ya kuomba ridhaa kwa Wananchi wamchague kuwa Diwani wa kata hiyo.
 Mgombea Udiwani wa Kata ya Vingunguti Kupitia Chama cha Mapinduzi , Omary Kumbilamoto  akiwa amebebwa juu juu na Mkada wa Chama Chake wakati akiwa anawasili kwenye uwanja wa Butiama Vingunguti .


 Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam akimwaga sera na jisni Ilani ya CCM inavyotekelezwa katika Serikali hii ya awamu ya tano
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakichea kwa pamoja mtindo wa Mduara wakati wa mkutano wa Kampeni za Udiwani kata ya Vingunguti

Wakazi wa Mtaa wa Butiama waliohudhuria Mkutanowa wa kampeni za udiwani za Omary Kumbilamoto

Mavunde afungua Maonesho ya kitaaluma ya chuo cha Mtakatifu Joseph

 Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde Akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph wakati wa Maonesho ya kazi zao za kitaaluma 
 Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akionyesha zawadi aliyopewa na Uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph wakati wa Maonesho ya kitaaluma
 Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akiagana  na wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph.
Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa katika picha ya Pamoja na Uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph 

Wednesday, August 29, 2018

PROF.NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Walimu wa Somo la Hisabati nchini  wanaongezeka hili kuweza kukidhi mahitaji ya walimu hao katika shule za Msingi na Sekondari.

Profesa Ndalichako amesema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la tano la Wakufunzi wa Hisabati kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan hapa nchini.

“Mkutano huu umekutanasha wataalamu kutoka Afrika na Nje ya Afrika kwa lengo la kuongeza jitihada za kuimarisha mbinu za ufundishaji wa Hisabati , hivyo tunataka kuongeza walimu wa hesabu hapa nchini lakini tumekuwa na upungufu wa vijana wanaomaliza elimu yao ya sekondari ambao ni wataalamu wa Hisabati hivyo nyie muende kuhamasisha vijana wakapende hesabu hili tuweze kupata mzunguko mzuri wa  wataalamu wa hesabu kila mwaka”amesema Ndalichako.

amesema hali ya uchache wa utayari wa vijana wanaojitokeza kuja kusoma hesabu imekuwa chanzo cha upungufu wa walimu wa somo hilo nchini hivyo Serikali ipo katika mpango kabambe wa kuhamasisha watoto wakasoma hesabu na kufanya vizuri katika masomo yao wakiwa darasani.

Waziri Ndalichako amesema kuwa ukiboresha ufundishaji wa somo la hesabu utasaidia kuboresha masomo mengine kwani masomo mengi yanategmea utalaamu wa hesabu kufanikisha ufaulu.

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kupokea maoni ni namna gani itaweza kuboresha mfumo wa utoaji wa elimu hasa kwa somo la hesabu hili kuweza kuongeza ufaulu katika shule za serikali.

Ametaja kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imeweza kuleta mfumo wa elimu bure kwa kutoa elimu ya kiwango cha hali ya juu na sio bora elimu hivyo walimu ni vyema wakathamini mchango unaotolewa na serikali ya awamu ya tano kwa wanafunzi kwa kumuunga mkono Rais wetu

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wataalmu wa somo la Hisabati katika kongamano la tano la Hesabu lililofanyika nchini nakuandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan 
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya magwiji wa Hesabau waliofika katika mkutano huo
 Washiriki wa Kongamano hilo wakipiga makofi kumpongeza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kumaliza kuzungumza
 Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Chuo Kikuu cha Agha Khan wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano hilo 

Tuesday, August 28, 2018

WATENDAJI HALMASHAURI YA MBEYA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUJITUMA


Na EmanuelMadafa,Globu ya JamiiMbeya
Watendaji wa Halmashauri ya Mbeya, wameaswa kufanya kazi kwa kujituma na kwa uadilifu mkubwa sambamba na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndugu  Stephan Katemba wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndugu Amelchiary Kuluzwira ambaye kwa sasa anaendelea na majukumu mengine.

Katemba, amesema hakuna sababu ya mtumishi kushindwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani wao ndio waajili wao wakubwa hivyo lazima kutekeleza hilo bila kuweka sababu.

“Sioni sababu ya mtumishi  kudai kwamba yeye hafungamani na upande wowote wakati anajua wazi kabisa serikali iliyopo madarakani imewekwa na chama cha mapinduzi hivyo utake usitake lazima utii hilo’ tena kwa uadilifu mkubwa,”Alisema Katemba

Amesema katika kutekeleza hilo yeye kama Mkurugenzi wa halmashauri atahakikisha analisimamia hilo  kwa vitendo kwani CCM ndio muajiri wake namba moja.

Amesema pamoja nakwamba kuna baraza la madiwani ambalo lina madiwani wa vyama tofauti lakini hata wao wanatekeleza Ilani ya CCM  kwani ndio serikali iliyopo madarakani .


Aidha Katemba ametoa wito kwa watumishi hao kuhakikisha wanalinda mfumo wa mawasiliano kati ya Idara na taasisi nyingine zilizoko nje ya halmashauri hiyo  na wanatakiwa watambue kuwa mtoa taarifa wa mwisho ni mkurugenzi na tayari amekwisha toa maelekezo hata kwa baraza la madiwani.

Kwa upande wake Mkurugenzi aliye maliza muda wake Ndugu Amelichiary Kuluzwela amewataka watumishi hao kuendeleza mazuei aliyofanya pamoja na kumpa ushirikiano wa kutosha mkurugenzi huyo mpya .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndugu  Stephan Katemba akimkabidhiwa  ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndugu Amelchiary Kuluzwira ambaye kwa sasa anaendelea na majukumu mengine.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndugu  Stephan Katemba akisaini Fomu za kukabidhi  ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndugu Amelchiary Kuluzwira ambaye kwa sasa anaendelea na majukumu mengine.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndugu  Stephan Katemba akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Ndugu Amelchiary Kuluzwira ambaye kwa sasa anaendelea na majukumu mengine.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo wakati wa makabidhiano ya ofisi.

DR.MPANGO AWAAGA WATUMISHI WATANO KUTOKA WIZARA YA FEDHA WANAOKWENDA KUSOMA UINGEREZA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango leo amewaaga watumishi watano wa wizara hiyo wanaosafiri kwenda nchini uingereza kwa ajili ya ufadhili wa Masomo uliotolewa na DFID Kupitia mfuko wake wa UKAID.

Akizungumza na Michuzi Media Group katika Mkutano wa kuwaaga watumishi hao Waziri Mpango aliwataka Vijana hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutokubali kuyumbishwa na jambo lolote la ujanja kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

“Hii nafasi niliomba mimi kwa ajili ya watumishi wa Wizara muende kujifunza na hili ni kundi la pili hivyo naomba mkafanye kile kilichowapeleka kwani watanzania Zaidi ya Milioni amsinii wanategemea kuja kunufaika na ujuzi mlioupata kutoka huku hili muweze kuja kuendesha tasisi hii ambayo ndio Ubongo wa uchumi wan chi yetu” Amesema Dr Mpango.

Amesisitiza kuwa yeye kama waziri anajivunia sana kuona Vijana wanapanua maharifa kwa kujiongezea elimu na maharifa kutoka sehemu nyingine kwani kunasaidia kujiamini na kuzungumza kwa hoja za uhakika mbele ya umati wa watu.

Amesema kuwa kama watalaamu wote hao kutoka wizara ya fedha watafanikiwa kufanya vizuri watazidi kuiongezea sifa nchi yetu kuendelea kupata nafasi ya kupeleka vijana wengi kwenda kujifunza.

Ameweka wazi kuwa yeye atakuwa Waziri mwenye furaha sana kwa kuona kila idara katika Wizara yake ina vijana makini ambao ni weledi katika kazi zao.

 Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango akizungumza na Vijana watano kutoka Wizara hiyo ambao wamepata ufadhili wa masomo nchini uingereza 
 Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango akisisitiza jambo kwa Vijana hao 
 Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango  akiagana na Vijana hao na kuwatakia Safari Njema
 Wafanyakazi wa Wizra ya fedha , Sudah Joseph, Peter Kalugwisha,Morick Mwasagwa,Eliud Mkilamweni na Tunsume Mlawa  wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango 
Waziri wa Fedha na Mipango , Dr Philip Mpango  akiwa katika picha ya Pamoja na Wanufaika wa Ufadhili wa Masomo wa DFID kupitia Mfuko wa UKAID

WAKUTUBI WAPATIWA MAFUNZO YA KUHIFADHI TAFITI KWA NJIA YA TEHAMA

 Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dr .Amos Nungu akizungumza na watalaamu wa Maktaba wakati akifungua mafunzo ya Tehama kwa wakutubi  kutoka tasisi mbalimbali nchini
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Biashara cha CBE , Profesa  Frolence  Luoga, akizungumza wakati wa Mkutano wa wakutubi juu ya masuala ya tehama katika kuhifadhi tafiti zinazofanywa hapa nchini na nje ya nchi kwa ajili ya kusoma.
 Sehemu ya Wakutubi walioshiriki  katika mafunzo ya kuhifadhi tafiti kwa njia ya Tehama wakisikiliza somo kwa makini
Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dr .Amos Nungu akiwa katika picha ya Pamoja wakutubi walioshiriki mafunzo ya tehama kwa ajili ya kutunza tafiti katika Maktaba

Monday, August 27, 2018

Vyama visivyokuwa na Ruzuku vyaitaka Chadema iache kuingilia wagombea wake.

Katibu Mkuu wa Chama cha AFP Taifa, Rashid Mohamed akizungumza na waandishi wa habari  kupinga Tamko la ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi wa Igunga na kutaka Chadema isiwaingilie kwenye maamuzi yao

NA Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Umoja wa vyama visivyokuwa na Ruzuku nchini ikiwemo chama cha AAFP, DP pamoja na Chama cha Demokrasia Makini wamelaani vitendo vya wagombea wa vyama hivyo kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kulalamikia tume ya uchaguzi kutotenda haki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge kwenye jimbo la Korogwe vijijini.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo, Katibu mkuu wa chama cha AAFP Rashid Mohamed Rai amesema kuwa baada ya kukagua fomu ya mgombea wa chama chake alibaini kuwa kuna baadhi ya tozo ambazo mgombea huyo alikuwa hajalipia licha ya kutumiwa fedha hizo na baada ya hapo akalalamika kuwa miongoni mwa watu ambao fomu zao hazijapokelewa wakati alikuwa hana vigezo na fomu yake ingekataliwa kwasababu hakulipia fedha za baadhi ya ada za uchaguzi.
“Kuna baadhi ya  magenge ya matapeli ambao wamevamia hivyi vyama kwa nia tofauti, kuna watu wanachukua fomu kwa nia ya kugombea wanaweka mfukoni halafu baada ya muda wanaanza kulalamika ukimwambia lete fomu uangalie unakuta yeye mwenyewe hakujaza fomu aliiweka tu” alisema
“Mfano mzuri ni Mgombea wangu, hata ile hela ya uchaguzi ya tume hakulipa halafu siku ya uchaguzi ananiambia fomu haipokelewi na mkurugenzi hayupo mpaka mida ya saaa 9 nauliza wenzake pale wananiambia bado mgombea huyo hajafika eneo la kurudisha fomu, anaingia pale saa 10 na yeye anaungana na hao wanaolalamika kuwa wamefamnyiwa ubaya” aliongeza Rai.
Amebainisha kuwa uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni tofauti lakini baadhi ya watu walikuwa wakidanganya ili kutengeneza mazingira ya kugombanisha tume na vyama vya siasa kwa nia mbaya, ambapo CHADEMA waliungana na Mgombea wao na kuanza kutumia maneno makali akilalamikia tume jambo ambalo ni uongo.
“Kama hata ada hakulipa lakini na eye anaungana kwenye mkutano wa  Chadema halafu anatoa povu hapo unajua kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwaambia wasirudishe fomu” aliongeza Rai kwenye taarifa yake
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mgombea wake majira ya saa saba akilalamika kuwa hamuoni mkurugenzi lakini baada ya hapo alikuja kupata kipande cha video ya mgombea wake akiwa kwenye ofisi ya Chadema akilalamika wakati CHADEMA haina mahusiano mazuri na chama cha DP.
“Sisi DP na Vyama wenza ambavyo havina ruzuku tutaungana  wakati tukienda kwenye uchaguzi wa Monduli kushiriki uchaguzi wa marudio lazima tupite korogwe tuonane na mkurugenzi tukajue tatizo lilikuwa ni lipi kisha tutatoa tamko pamoja au chama kimoja kimoja” alisema Mluya
Aidha amebainisha kuwa  kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwapigia simu wagombea wa vyama hivyo wanaoshiriki uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Monduli, wakiwatishia na kuwaambia wajiunge na vyama vyao na wawaunge mkono na kusema kuwa vyama hivyo vitaenda kushughulika na kuhakikisha wanakabiliana na watu hao wenye nia mbaya ya kugombanisha tume na Vyama Vyao.

KESI YA KINA MBOWE NA WENZIE YARUSHWA MPAKA SEPT 27 MWAKA HUU

NA EUNICE SHAO

Kesi dhidi ya vongozi tisa wa  (Chadema) akiwamo Freeman Mbowe wanaokabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  itatajwa Septemba 27, 2018

Washtakiwa walipaswa kusomewa Maelezo ya awali leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini imeshidikana kwa sababu mshtakiwa wa tano, Esther Matiko hakuwepo mahakamani na mdhamini wake alieleza kuwa anatatizo la kiafya kwenye mfumo wa uzazi.


Pia  Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliieleza  mahakama kuwa mshtakiwa Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa Iringa mjini alikuwa akitetewa na wakili Jeremiah Mtobesya ambaye amejitoa.

Aidha, mshtakiwa Peter Msigwa aliiomba Mahakama kuandikia hati ya wito (Summons) Mahakama ya Iringa kwa kuwa muda mwingi yupo katika Mahakama ya Kisutu na yeye bado ana kesi kwenye mahakama hiyo.

Pia ameiomba mahakama impatie  muda wa wiki tatu ili aweze kutafuta wakili mwingine,

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Mbali Mbowe na Msigwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

MAHAKAMA TIDO MHANDO ANAKESI YA KUJIBU KATIKA MASHTAKA YANAYOMKABILI

NA EUNICE SHAO


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 27, 2018  imemkuta Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka ta matumizi mabaya ya madaraka ana kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuleta mashahidi watano.

Hakimu Shaidi amesema, amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 27, 2018  imemkuta Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka ta matumizi mabaya ya madaraka ana kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuleta mashahidi watano.

Katika kesi hiyo Tido anakabiriwa na
mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.

Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya;  mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008,  akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Tido  ambay anatetewa na Wakili Ramadhani Maleta na yupo nje kwa dhamana ataanza kujitetea Septemba 20.2018

Katika kesi hiyo Tido anakabiriwa na
mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.

Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni, ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya;  mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008,  akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BV

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...