Saturday, September 15, 2018

POLEPOLE AHITIMISHA KAMPENI ZA UDIWANI VINGUNGUTINa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Kampeni za  udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikatetamaa, ambapo pole pole alikuwa mgeni rasmi nakuwaeleza makutano hao kuwa chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dr John Pombe Magufuli kimefanikiwa  mambo mengi ya maendeleo  ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za msingi.


 "Watu wenye akili zao vijana na kama Kumbilamoto na akinamama mtatiro wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono Rais, nami na waaomba  kesho siku ya jumapili tarehe16/2018 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said Kumbilamoto mapematu tuwetumeshinda Jina lake kwenye karatasi litakuwa nambambili"amesema


 Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea, Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF  na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.

Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura kwa wingi iliaendeleekuwatumikia  akiwa CCM na kuwaletea maendeleo.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwisho wa Kampeni za Mwisho Udiwani kata ya Vingunguti
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Humphrey Polepole akimnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Vingunguti Kupitia CCM , Omary Kumbilamoto
 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Vingunuti Omary Kumbilamoto akiomba Kura kwa mara ya mwisho wakati w akuhitimisha kampeni
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo kupitia  Chama Cha Wananchi CUF ,Sharifu Mbulu akizungumza mara baada ya kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni Vingunguti
 Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza Jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika Mkutano wa kuhitimisha Kampeni Vingunguti
 Aliyekuwa Diwani wa Mtoni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam , Benard Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano wa kuhitimisha Kampeni kat aya Vingunguti
Friday, September 14, 2018

TAKUKURU YAWASAKA HANSPOPE NA LAWUO KWA KOSA LA UDANGANYIFU


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana  na Rushwa (TAKUKURU) inawatafuta  washtakiwa, Zacharia Hanspope ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya Simba Sports Club na ndugu Franlin Peter Lauwo ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ranky Infrastrure  & Engineering  iliyopewa zabuni ya kujenga uwanja wa Simba kujibu kesi ya jinai namba 214/2017.

Akizungumza na Waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo amesema  Mshatakiwa wa kwanza, Zacharia Hanspope aliondoka nchini mnamo April 8 ,2018 kupitia mpaka Horohoro kwa kutumia Passport namba TA00422.

“Mfanyabiashara aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ambaye alizaliwa Iringa Mjini ambaye kabla ya kuondoka alikuwa anaishi Mlalakuwa Mikocheni ambaye amebainika kuwa anamiliki hati za kusafiria tatu ambapo moja ni hati ya kusafiria ya Afrika Mashariki na hati mbili za kusafiria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotolewa kwa vipindi viwili tofauti ambapo hati ya kwanza yenye nambari AB710516 ya 16 April 2016 na nyingine ni hati yenye nambari AB 92 9732 Iliyotolewa tarehe 16 Novemba 2017”amesema

Amesema kuwa mshatikiwa namba moja anashtakiwa kwa kwa kosa la kutoa taharifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi K/F106(1)(A)&(C) Cha kodi ya mapato chini ya sharia ya kodi namba 332.R.E 2008  kwamba kati ya washtakiwa wenzake Evans Aveva na Godfrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania .

Amesema kuwa maelezo hayo yalikuwa kwamaba Simba Sports Club wamenunua nyasi za Bandia kutoka kampuni ya Ninah Guanzhou Trading Limited kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577.00 USD , Maelezo ambayo yalikuwa ya uongo kwania nyasi hizo zilinunuliwa kwa 109,499.00 USD.

Generali Mbungo alimtaja ndugu Franklini Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi bila ya kusajiliwa K/F22(1)(D) Cha usajili wa wakandarasi Sura ya 235 ya 2002 Kwamba kati ya Machi 2016 na Septemba 2016 Mshatakiwa alifanya kazi za ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba Sports Club Uliopo Bunju Manispaa ya Kinondoni kwa thamani ya Tsh 249,929,704  wakati akiwa ajasaliwa katika bodi ya wakandarasi Tanzania hivyo kisheria alikuwa haruhusiwi kufany akazi hiyo.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...