Saturday, October 13, 2018

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUWA WAADILIFU


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya Tasisi za Umma kuendelea kufanya Vibaya  katika maeneo ya Ununuzi na Ugavi hili hali bodi ya usimamizi wa masula hayo ipo.
Naibu katibu Mkuu amesema hay oleo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa Mahafali ya tisa ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“ninawaagiza kwa kushirikiana na tasisi zingine zinazosimamia ununuzi wa Umma kama  PPRA,GPSA,PPAA na zingine mlete mpango kazi namna mtakavyofikia tasisi za umma ili kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tuweze kutekeleza jambo hili mapema iwezekanavyo.Lengo ni kuhakikisha tunatumia rasilimali zilizopo ili kuleta Matokeo Makubwa kwa Wananchi” Amesema Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, Godfred Mbanyi  amesema bodi itaendelea na jitihada zake kuhakikisha wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa stahiki ili kuweza kupenya na kuleta ushindani katika soko la ajira la ndani nan je ya nchi .

Mbanyi amesema bodi imeweza kuwatafutia fursa vijana wawili wa CPSP Na Wanafunzi bora wa somo la Procurement and Suply Audit nafasi ya ajira katika tasisi ya Kimataifa ya Nexia SJ Tanzania ambao ni Wataalamu wa Ukaguzi, Hesabu,Kodi, Ushauri wa Kibiashara nk.

Mbanyi alimaliza kwa kutoa rai kwa wahitimu wote watakaotunukiwa shahada ya juu ya fani ya ununuzi na ugavi wafanye hima kujisajili na bodi ili waweze kufanya kazi za ununuzi na ugavi kihalali na kwa mujibu wa sheria .

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akihutibia wakati wa mahafli ya tisa ya Bodi ya Wataalmu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi , Godfred Mbanyi akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya tisa ya bodi hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi wa Ugavi SR.DKT.Hellen Bandiho akizungumza katika mahafali ya tisa ya bodi yake yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban  akikabidhi cheti kwa Mwanafunzi Bora wa mahafali hayo ambaye amefanya vyema kwenye tafiti yake.
 Bahadhi ya Wahitimu wakiwa wamekaa wakisubiri kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
 Wahitimu wakiwa wamekaa wakisubiri kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
 Wahitimu wakila kiapo cha Uadilifu na Maadili mbele ya Mgeni rasmi mara baada ya  kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa bodi hiyo

Thursday, October 11, 2018

MSICHANA INITIATIVE YAHADHIMISHA SIKU YA MSICHANA DUNIANI

 Muwakilishi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Eugine Shao, akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa kuhadhimisha siku ya Msichana Duniani na Malengo ya Tasisi yao katika kumlinda Mtoto wa Kike hili aweze kufikia malengo sanjari na kupata elimu.
 Mourine Richard Kutoka Tasisi ya Her Initiative akkizungumza umuhimu wa Mtoto wa kike kujiamini na kuwataka wanaume kuondoa dhana ya kuwanyanyapaa Wanawake kwa umri.
 Dada Viola akitoa mada kwa wasichana waliohudhuria kongamano katika kuhadhimisha siku ya Msichana Duniani kwa kuwataka waweze kujiamini.
 Mmoja wa wadau walioshiriki katika Kongamano la siku ya Msichana Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wasichana walioshiriki katika Kongamano siku ya Msichna Duniani katika Ukumbi wa Nafasi Arts Space.

NAIBU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI ATAKA WANAOPINGA MUUNGANO WASHTAKIWE KAMA WAHAINI


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed ametaka kutungwa kwa sharia Maalum kwa watu watakaobeza Muungano kutajwa kuwa ni wahaini.

Ahmed Amesema hay oleo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akichangia Mada katika kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililobebwa na Mada ya ‘Falsafa ya Mwalimu Nyerere juu ya Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda Tanzania’.

“mimi ninachoomba tuvutane tu ila tuwandalie mstakabali mzuri hao wanakuja nyuma yetu na tuwajenge hawa kwa mazuri nimeguswa kidogo na katibu wa baba wa Taifa pale alipouliza nyie vipi huko katika vyama vya siasa nimekuwa nashangaa sana wanasiasa awajui kupambanua kipi cha kubeza na kipi sio cha kubeza”

Ahmed amesema kuwa kuna tatizo la kisheria katika mfumo wa kuongoza hivi vyama kwani wanasiasa ndio wamekuwa kipaumbele kuhoji muungano jambo ambalo linafanywa kwa utashi wa kulenga kupata kura tu.

Amesema ifike wakati wakusema kuwa mtu akigusa Muungano ni uhaini sio kwa kumgusa Rais Peke yake kwani wanfanya hivi kwa kutaka kupata umaharufu wa kisiasa.

Amesema ifike mahali ni sharia kufata fikra za Mwalimu kwani anayekiuka hizo atakuwa ametenda kosa kubwa la jinai kwani tukiacha uhuru tutaendelea kudanganyana siku hadi siku.
Alimaliza kwa kusema kuwa leo amekuja Rais Dk John Magufuli anasimamia haya lakini ipo siku atakuja kiongozi atayaaopuuza haya anayofanya kisha taifa hili litapromoka kwa kiwango cha ajabu nakupoteza nguvu yote hii.
 Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa mada ya Umuhimu wa Taifa huru na uhuru wa Wananchi katika kukuza uchumi wa Viwanda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigambboni Sarah Msafiri akizungumza kuhitimishaKongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere
 CAG Mstaafu, Ludovick Utouh akichangia mada katika Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Watoa mada na Wajumbe wa Meza kuu wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Viongozi wastaafu na wadau mbalimbali wakifatilia kwa karibu Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
Picha ya Washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam

RC MAKONDA ATEMBELEA KIMARA NA KUJIONEA CHANGAMOTO ZA MRADI WA DART

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa Kimara mara baada ya kutembelea kituo cha Mabasi ya Mwendokasi na kujionea kero na changamoto za mradi huo na kuaidi kwenda kuzungumza na Waziri wa Tamisemi, Suleimani Jaffo hili waweze kutatua kero hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda  akitembelea eneo la kituo na kujionea Changamoto zilizopo
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda , akifungua geti lililofungwa  eneo la Kimara Mwisho Wananchi wasipite na kuamuru litumike kuanzia leo hili kiupunguza kero kwa Wananchi
 Wananchi waliokuwa wamefurika eneo la Kimara kusubiri Mabasi ya Mwendokasi
 Abiria wakiwa wamebanana  ndani ya basi la Mwendokasi  kutokana na uchache wa mabasi
 Wakazi wa Mbezi na Kimara wakiwa wamejazana kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam eneo la Kimara Mwisho

Wednesday, October 10, 2018

WAZIRI NDALICHAKO SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE YOTE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Waziri wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi, Prof.Joyce Ndalichako 
amesema falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zimepata msukumo wa hali ya juu katika serikali ya awamu ya tano kwa kuwataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.

Prof Ndalichako amesema hayo leo Mapema Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la Siku mbili katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam lililokuwa na Mada inayosema  'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

"Mwalimu Nyerere alisisitiza kufanya kazi kwa bidii na udalifu na kusimamia msingi wa uzalendo kwani Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dk. John Magufuli ameweza kusimamia neno la hapa kazi tu ambalo ni moja ya Falsafa ya Mwalimu Nyerere iliyosema kuwa kufanya kazi kwa bidii , Kazi ni Uhai na Kazi ni Utu hivyo tunapaswa kujiuliza hii falsafa ina umuhimu gani katika kufanikisha kuelekea uchumi wa Viwanda"

Prof Ndalichako amesema kuwa kuna mambo mengi yanafanywa na Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuyafanya ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa wa Mwalimu Nyerere hivyo hii falsafa iweze kuangaliwa ni namna gani itaweza kuleta mchango wa Maendeleo ya Viwanda katika Taifa hili kwani mada iliyochaguliwa ina akisi msisitizo wa serikali yetu.

alisema kuwa nia ya Serikali ni kuendeleza miradi Mikubwa ambayo ndio Msingi wa kufikia Maendeleo ya Haraka kama ujenzi wa mardi mkubwa wa umeme wa Stiglizers  gorge ambao utasaidia kuzalisha umeme mkubwa katika nchi hii  ambayo ni Nishati Muhimu

alimaliza kwa kuwataka watanzania kuunga mkono Juhudi za Rais wetu ambaye amekuwa kipaumbele katika kusimamia rasilimali za Taifa hili tuweze kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati hivyo waswahili usema 'penye nia pana njia'
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Prof ,Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamno la Kumbukumbu la kuenzi kazi zilizofanywa na Mwalimu Nyerere lilikuw ana kichwa cha Habari cha 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,Mashavu Fakih akizungumza kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi
 Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila akizungumza na watu waliofika katika kongamno hilo.
 Baadhi ya Viongozi Wastaafu walioshiriki katika Kongamano hilo la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dr .Bashiru Ally Bashiru akifatilia Mdahalo wa 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda' uliofanyika katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Magogoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...