Thursday, February 21, 2019

GLORY MZIRAY AAGWA DAR NA KUSAFIRISHWA KWENDA MOROGORO

 Mume wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja wa Uhusiano Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Akiwa na Watoto wake wakitoa Heshima ya Mwisho kwenye ibada ya kuaga Marehemu huyo katika Kanisa la KKT Usharika wa Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam ambapo Marehemu amaeagwa hapo na wakazi wa Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mikese Morogoro.
 Wahubiri wakitoa Baraka na Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Glory Mziray ambae alikuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
 Watoto wa Marehemu Glory Mziray wakiongoza mbele na Msalaba wakati wakiondoka Katika Kanisa la KKT Usharika wa Mbezi Beacha Kuelekea Mjini Morogoro.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Dk Mary Mwanjelwa aktoa Salamu Kabla ya kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) ,Dk.Mwanjelwa amezungumzia jinsi alivyo mfahamu Mziray tangu alipokuwa nae katika Chuo kikuu cha Mtakatifu agustino na kutaja umhiri wake katika kutimiza wajibu na majukumu anayopewa.
 Mkurugenzi wa Huduma za Misitu ,Emmanuel Willfred, akizungumza na kutoa wasifu wa Marehemu Glory Mziray enzi za uhai wake katika eneo lake la kazi kama Meneja wa Mahusiano.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAID'S),Fatuma Mrisho akizungumza juu ya uzoefu wake katika kazi na Marehemu Glory Mziray.

 Sehemu ya Wafanyakazi wa TFS wakitoa heshima za Mwisho kwa Marehemu Glory mziray
 Sehemu ya Watu mbalimbali waliojitokeza kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray katika ibada iliyofanyika katika kanisa la KKT Usharika wa Mbezi Beach.

No comments:

Post a Comment

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...