Saturday, June 15, 2019

Zaidi ya washindi 2000 kunufaika na adhimisho la miaka mitano ya M-Pawa ya CBA na VODACOM


.

CBA na Vodacom leo wamefanya droo ya kwanza kwa ajili ya promosheni ya kutunza na kulipa madeni wakisherehekea miaka 5 ya huduma ya M-Pawa yenye lengo la kuongeza uhusisho wa watu kwenye huduma za kifedha na kuhimiza tabia ya kutunza kwani ndiyo lilikua dhumuni la msingi toka M-Pawa ilivvoanzishwa. 

Promosheni hii inayokusudiwa kufanyika kwa muda wa wiki 6 imeanza na droo ya kwanza ambayo itatoa jumla ya washindi 340 ambao 40 kati yao wataondoka na mara mbili ya fedha waliyohifadhi kwenye akaunti zao kuanzia kiasi cha Shilingi 1000 – 200,000 na wengine 300 kushinda vocha ya shilingi 5000 kila mmoja. Promosheni hii itaendelea kila wiki huku kukiwa na washindi wengine 50 wa kila baada ya wiki 2 ambao watashinda zawadi ya simu na mshindi mkubwa ambaye atatangazwa kwenye droo ya mwisho ya promosheni hii atakayezawadiwa kiasi cha milioni 15.

Washindi watachaguliwa kutokana na vigezo viwili ambavyo ni shindano la kutunza fedha na shindano la kulipa deni ambapo mtu yeyote mwenye akiba ya kuanzia Sh 1000 mpaka Sh 200,000 atapata mara mbili ya hela yake na wenye hela zaidi pia watapata Sh 200,000 katika droo za kila wiki pamoja na zawadi nyinginezo.

Akiongea kwenye droo ya kwanza CEO wa CBA benki bwana Gift Shoko alisema  “M-Pawa ni huduma ambayo inaendelea kuwawezesha watanzania wengi hususani wafanyabiashara wadogo na tunaadhimisha miaka 5 kwa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma hii. Tunaendelea kuhimiza kutunza na kulipa madeni mapema na kuhamasisha watu wasiotumia M-Pawa kuanza kuitumia huduma hii”

Aliendelea kuwahimiza wateja kujiunga katika promosheni kwa kuwa itawapa nafasi ya kuweza kufanikisha ndoto zao iwapo watashinda. Aliendelea kwa kuwaomba wateja kuwasiliana na huduma kwa wateja ya CBA wakiwa na maswali yoyote kuhusu promosheni au kusoma habari, mabango pamoja na kufuatilia kurasa za kijamii na tovuti za CBA/Vodacom. 

Droo ya kwanza ilifanyika kwenye makao makuu ya benki ya CBA jijini Dar es Salaam na ilisimamiwa na wawakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bwana Humudi AbdulHussein Alisa Mwandamizi Mkaguzi pamoja na waakilishi kutoka CBA Tanzania.  


Thursday, June 13, 2019

Bil. 32.5/= kuipamba bandari Kigoma, Ujenzi wa Gati la Ujiji na Kibirizi waanza kwa kasi


Na Humphrey Shai, Globu ya Jamii, Kigoma.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa Sh bilioni 32.5 kwajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa gati katika bandari ndogo za Ujiji na Kibirizi zilizopo Kigoma mjini.
Pia mradi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la gorofa moja kwaajili ya ofisi za meneja wa bandari za ziwa Tanganyika.
Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya China Railway 15 Group ulianza Februari 28, 2018 na unahusisha ujenzi wa gati la Kibirizi lenye urefu wa mita 250 na kuifanya bandari hiyo kuwa na gati refu kuliko bandari zingine katika Ziwa Tanganyika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ndogo ya Kibirizi, Afisa Bandari hiyo, Ghalib Mahyolo, alisema kwa sasa licha ya kutokuwepo kwa gati la kisasa wanahudumia tani 600,000 hadi 700,000 kwa mwezi.

Pia alisema kwa mwezi mmoja wanahudumia boti zipatazo 220 hadi 260 na boti 70 kati ya hizo ni za abiria ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 50.

Alisema boti za abiria zinahudumia vijiji vitatu ambavyo ni Kagunga, Mwamgongo na Mtanga ambapo usafiri unapatikana siku zote za wiki isipokuwa Jumapili.

Kwa upande wa uwezo wa boti za mizigo zinazohudumiwa bandarini hapo alisema boti kubwa kabisa zina uwezo wa kubeba tani 120 na zinafanya safari katika ya Tanzania, Burundi na DRC.

"Mradi wa kujenga gati mpya hapa Kibirizi utaongeza biashara ya usafirishaji wa mizigo na abiria kwani itawezesha upakiaji na upakuaji kufanyika kwa urahisi zaidi tofauti na ilivyo sasa," alisema Mahyolo.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, alisema mradi huo ni mkakati wa TPA kuboresha bandari ndogo za maziwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma pamoja na kuongeza mapato.

Msese alisema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa uzio kuzunguka bandari ya Kibirizi ambayo imekuwa na changamoto yakuingiliwa na shughuli zingine za wananchi ambazo si za kibandari ikiwemo kuchota maji katika eneo la bandari.

Alisema pia kutakuwa na ujenzi wa jengo la abiria, ghala la kuhifadhia mizigo, vyoo na kibanda cha mlinzi pamoja na uwekaji wa paving.

Akizungumzia mradi huo Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji wa Maboti, Edmond Msabaha, alimshukuru Rais John Magufuli kwa serikali kuptia TPA kuona umuhimu wa kuwajengea gati ku wa la kisasa.
Alisema kwa sasa wanapakiza mizigo na abiria kwa shida tofauti na ikiwepo gati la kisasa.


"Mradi hii utakua na manufaa kwetu wasafirishaji na hata wateja wetu lakini pia utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kutokana na kazi kuwa zinafanyika kwa haraka, hivyo nimshukuru Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu," alisema Msabaha.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Mseseakizungumza juu ya kazi zinazofanywa katika Bandari ya Kigoma na Miradi itakayojengwa katika bandari hiyo
 Moja ya Mashine iliyopo katika Bandari ya Kigoma inayonyanyua  mizigo kwa haraka ambapo bandari hiyo inaborehsw akwa gharama ya zaidi ya Milioni 30.

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...